TANGAZO YA NOELI:LEO ANAZALIWA MWOKOZI ambaye ndiye Kristo Bwana

24 décembre 2009

Evangile

natalesuore1.jpg

 Enjili ya Mt. Luka : 2,1-14

 1Siku zile Kaisari Augusto, mtawala wa milki ya Kirumi, aliamuru ya kwamba watu wote wa milki yake waandikishwe. 2Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza kufanyika nayo ilitokea wakati Kirenio alipokuwa liwali wa Siria. 3Watu wote walikwenda katika sehemu walikozaliwa ili waandikishwe huko. 4Yusufu alitoka mji wa Nazareti uliopo Galilaya akaenda mpaka Bethlehemu mji wa Daudi kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi. 5Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na mchumba wake Mariamu ambaye kwa wakati huu alikuwa mja mzito.

 6Walipokuwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu kujifungua uli fika, 7naye akamzaa mtoto wa kiume, kifungua mimba. Akamfunika kwa vinguo na kumlaza horini, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.

 8Usiku ule walikuwako wachungaji wakilinda kondoo zao nje ya mji. 9Rafla, malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Mungu ukawang’azia pande zote. Wakajazwa na hofu kuu. 10Lakini malaika akawatuliza akisema: « Msiogope! Nawaletea habari njema ya furaha kubwa, na habari hii ni kwa faida ya watu wote! 11Kwa maana leo katika mji wa Bethlehemu, amezaliwa Mwokozi ambaye ndiye Kristo Bwana. 12Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa vinguo na kulazwa horini. »

 13Mara jeshi kubwa la malaika wa mbinguni likatokea na pamoja wakamsifu Mungu wakiimba: 14 « Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwepo amani kwa watu ambao amependezwa nao. »

Ndugu  na dada hamujambo wote.

Baraka na amani ya Mwenyezi Mungu na ya siku kuu ya Noeli iwafikie popote mulipo na katika shida zote za maisha yenu.

Tunafika ku Noeli ya mwaka elfu mbili na kenda.  Tunafika mara ingine mwaka huu pangoni mwa betlehemu kwa kuona mambo ya ajabu ambaye Mungu Baba ametutendea sisi wanadamu wa kila nyakati na wa kila nafasi.

Noeli ni nini?

Noeli ni kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu wa Nazareti hapa duniani.  Lakini si yote, kwani inatufaa kabisa kujua yote kuhusu huyu Yesu wa Nazareti,  na kujua sababu gani huyu Yesu wa Nazareti anafika hapa duniani kama vile mtoto mchanga.

Huyu Yesu ni mwana wa Mungu, nafsi ya pili ya Utatu mtakatifu, ni Mungu yeye pia.

Mungu Baba, katika mapendo na huruma yake amekusudia kumrudishia mwanadamu, aliye anguka katika zambi ya  kumkosesha katika mpango wake, na Kama vile Baba mwema, ku mtuma mwana wake wa pekee hapa duniani, ili akomboe dunia , ndiyo kutukomboa sisi wanadamu wenyi zambi na kuturudishia uhuru na haki, na ubora wa hali ya kimutu.

  Noeli jana

Tumesikia enjili.  Wakati wa Kaisari Augusti, Maria na Yosefu wanaenda kujiandikisha pa Betlehemu, kwani Yosufu alikuwa wa ukoo wa Daudi, ndiyo mwamemba wa jamaa ya Daudi. Basi pale Maria anatimiza siku za kuzaa, na anazaa mtoto wa kiume, naye ndiye huyu Yesu wa nazareti. « Akamfunika kwa vinguo na kumlaza horini, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni. » 

Leo duniani, Noeli ni nini ?

Leo Noeli ni wakati wa zawadi, wa mapumziko, wa siku kuu, wa chakula, wa furaha.  Tunapita katika siku hizo mgini mwetu tuonaona kabisa kama  watu wanatangatanga kabisa katika duka mbalimbali ya kila haina kwa kutafuta zawadi ya kutolea kiisha kwa wajamaa na marafiki. Noeli ndiyo inanafananishwa na zawadi.  Katika inchi zilizo endelea, kama vile ulaya na marekani tunaweza pia kuona watu wakijiandaa namna zote, barabara zinapambwa kwa namna ya kipekee, miti inayo itwa ‘’sapins’’zinatiliwa katika nyumba nyingi, wazazi wanatolea watoto wao zawadi mbalimbali na watu wafurahi wakila na kunya kwa namna ya kipekee. Tunaona kama hiyo ndiyo namna wanadamu washerehe noeli siku za leo na mara nyinigi hali ya ki kristu inatiwa pembeni na noeli inakamata sura ya kidunia…

Na kwa sisi wakongomani wa leo, Noeli ni nini ?

Wakongomani wote, wenye kukaa nchini. Lakini wale pia wanaokaa pembeni katika nchi za kigeni, wenye kuitwa “diaspora”. Noeli inapshwa kuwa Noeli ya matumaini. Matumaini ya amani, matumaini ya usalama, matumaini ya kuishi vizuri bila kutangatanga ao bila woga, matumaini kuishi bila njaa, matumaini yakukomeshwa vita na miliyo ya silaha, matumaini ya kuona wakimbizi wanarudia vijijini mwao na kurudilia shuruli zao za kawaida wakilima shamba zao, matumaini kwa mama kutokubakwa na tendeza ujeuri tena, matumaini ya kuishi katika haki na sheria.

Wandugu na wadada wengi, wa baba na mama na hasa wazee na wototo wengi wanasumuliza na kuteswa sana. Siku hizi kama vile ngambo ya Beni Lubero, Walikale, Masisi, Rutshuru, na tangu siku za nyuma nyuma huko ngambo ya Equateur. Wajeuri na majambazi, maaskari wa inchi (FARDC) wanasumbua watu na kuwatesa sana, watu wanauwawa sawa nyama za pori, umutu hauna tena fasi yake, mtu anatiliwa ku namba ya nyama na kutendewa kipagani ovyo katika mateso nyingi sana. Mama zetu, dada zetu na mabinti wetu wanazarauliwa na kutendewa unjeuri usio kuwa ka kipimo, wanabakwa ovyo na kuambukiziwa na magonjwa ya kila namna kama vile ukimwi na virusi mbalimbali. Watu wanapoteza hamu yote ya kuishi na ya maisha.

Jimboni kivu ya kusini kwa jumla na katika muji wetu wa bukavu kwa upekee, ujeuri na usalama mudogo unazidi kuonekana. Watu wanauwawa kila siku kwa pigwa risasi na watu wenyi kuvaa vazi la kiaskari na kumiliki silaha. Wanamungambo wa FDLR wanaendelea kutesa raiya wa kichoma vijiji, wakipora mali na ufugo na wakiuwa ovyo na kubaka wa mama. Na mwisho pa Bukavu: Abbé Daniel na Soeur Denise waliuwa. Katika Noeli huu naomba wakubwa wetu wa nchi wafungue macho na masikio , wasikie malamiko ya watu, waone damu ya wandugu wao. Na wakamate madaraka zao bila kusita ao kusema ovyo, ili yote iweze kuishi.

Ni sauti ya yule mtoto mwenye kuwa pangoni mwa Betlehemu: «  Leo Ni Noeli, uangalie na macho wale wadugu wenye kuteshwa ovyo, usiwe mukaramusi na mwenye kiburi. » Tusikie leo siku ku ya Noeli, matangazo ya malaika wenye kuimba mbinguni katika katikati ya usiku huu : « Sifa kwa Mungu mbinguni na amani duniani kwa watu wa mapenzi mema. »

Akina Bwana Presidenti, Akina Bwana mkubwa wa Gouve nement: mukitaka amani, munaweza kuwa na amani. Kwani yote inaweza kutoka kwa mapenzi yenu. Na amani nchini mwetu hapa mu Kongo inajengwa tu pamoja na Bwana Yesu, yeye mkubwa wa amani.  “Heri kwa wale wote wanaopenda kujenga amani…” Munauweza, ila inawakosa tu nia nzuri na huruma.

Ndiyo Noeli ya kusikia malamiko ya watu wenye kuteswa kwa njaa, kwa vita na ujeuri, kwa silaha, na hasa kuteswa ya kuona kama nchi inaendela kuwa na magumu zaidi na zaidi na viongozi wetu wanashindwa kufanya lolote kusudi wanainchi waishi katika hali bora ya amani na maendeleo.

Kwa noeli ya mwaka huo tunaomba wakuu viongozi kusikia malalamiko ya wanainchi na kutafuta kwanza faida ya wa congomani wote na kutiya faida yao binafsi nyuma.

Enyi wakuu viongozi, muwe na moyo ya huruma na musikiye kilio ya wana wa congo, magumu inapita, watu hawana mushahara, vijana hawapati kazi, njia zinakufa zote, watoto hawasomi na matunzo inakua shida na tatizo kubwa sana…Basi nawasihi, nyinyi wakuu viongozi, munao jiita wa kristu, ukristu wenu usiwe wa jina tu, ila wa matendo mukitafuta maendeleo na hali bora ya wa congomani wote.

Kwa noeli hii ya 2009 Mwenyezi Mungu na yeye KRISTU MKOZI NA MUKOMOZI WETU awakute na mukubali kusikia malalamiko ya wana wa congo na badilike mwenendo wenu kwa manufaa ya wa congomani wote na ndipo mutaitwa waana wa Mungu na huyu atawabariki na atabariki inchi yetu ya Congo.

Ndiyo Noeli yetu itakuwa Noeli ya kweli.

Maatakio mema kwa wote ili Noeli ya 2009 iwaonyeshe kabisa njia ya kuwa na amani na kuishi katika ubora na katika hali ya kibinadamu kama vile watu uhuru na wa kweli.

NOELI NJEMA, NOELI YA MALAMU, NOELI IYELEGELA, NOELI BWACHI, NOELI NINJA BWENENE BWENENE, NOELI BISOKA…….

Na tuende sasa sisi zote Bethlehemu, tuone mambo ya ajabu, na tupokee katika roho na maisha yetu wokovu wa Mungu. Muwe mwangaza na chunvi ya dunia ili watu wote wautukuze MUNGU na wa musadiki kama bwana na mokozi wetu, yeye aliye muleta amani.

Nakushukuru, ee Bwana, kwa mema yote ulisha na utakayo endeleya kutendeya katika maisha yangu yote. Amen

Nawasalimu nyingi wote. Mungu awabariki, awalinde, awape nguvu ya kumkuta na kumfuata. Aksanti na salamu kwenu wote.

© kakaluigi, Noeli 2009

À propos de kakaluigi

Agé de 66 ans, avec 35 ans passés en Afrique dans la République Démocratique du Congo comme missionnaire. Engagé dans l'évangélisation, le social et l'enseignement aux écoles sécondaires. Responsable de la Pastorale de la Jeunesse, Directeur du Bureau Diocésain pour le Développement (BDD), Directeur d'une Radio Communnautaire et membre du Rateco.

Voir tous les articles de kakaluigi

Inscrivez vous

Abonnez-vous à notre newsletter pour recevoir les mises à jour par e-mail.

Pas encore de commentaire.

Laisser un commentaire

Vous devez être Identifiez vous Poster un commentaire

carrosserieautopro |
ThinkBlog |
Dipersés... fRaNce aMéRIqUe... |
Unblog.fr | Créer un blog | Annuaire | Signaler un abus | madame dousse
| Les diplomes du club
| blog de jiji22